UKARABATI VIVUKO MV. KIGAMBONI NA MV. PANGANI II WAENDELEA KWA KASI
Posted On: September 15, 2026
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Mhandisi Lukombe King’ombe ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa vivuko MV. KIGAMBONI na MV. PANGANI II vinavyoendelea kufanyiwa ukarabati mkubwa katika yadi ya Songoro Marine Transport Boatyard iliyoko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Vivuko hivyo viwili ni MV. KIGAMBONI kinachotoa huduma kati ya Magogoni Wilaya ya Ilala na Kigamboni Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam pamoja na MV. PANGANI II Kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni, Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga na Serikali imeamua kuvifanyia ukarabati mkubwa ili kuboresha utoaji wa huduma katoika maeneo vinapotoa huduma.
Ukarabati wa vivuko hivyo viwili na vingine kote Nchini unafanyika ukiwa unalenga kuboresha na kuimarisha usafiri wa maji, usalama wa vyombo vya maji, ufanisi na upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za usafiri wa maji kwa wananchi wa Tanzania.