TEMESA, AFRICARRIERS WAFANYA KIKAO CHA MASHIRIKIANO
Posted On: September 23, 2026
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umefanya kikao cha mashirikiano ya kimkakati na kampuni ya AFRICARRIERS LIMITED kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ufundi na matengenezo ya magari nchini. Kikao hicho kimefanyika Septemba 22, 2026, katika Ofisi Makao Makuu ya TEMESA, jijini Dodoma.
Tasisi hizo zimejadili maeneo ya ushirikiano ikiwemo kubadilishana utaalamu, teknolojia na kuongeza ujuzi wa wahandisi na mafundi wa TEMESA, hususan katika mifumo ya kisasa ya magari na teknolojia za kidijitali za uchunguzi na matengenezo.
Ushirikiano huo unalenga kuongeza ufanisi wa huduma za matengenezo ya magari, kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza matumizi ya teknolojia, huku ukiimarisha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika maendeleo ya sekta ya magari nchini.