WAJUMBE WA BODI YA USHAURI TEMESA WAKAGUA MIRADI

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA wamekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/2020 ikiwemo ujenzi na ukarabati wa ofisi ya meneja na karakana ya Vingunguti mkoa wa Dar es Salaam, ukarabati wa kivuko cha MV. Kigamboni, upanuzi wa banda la abiria Kigamboni pamoja na ununuzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati