WAZIRI KAMWELWE AWAFUNDA MAMENEJA TEMESA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe leo amefanya kikao na menejimenti ya TEMESA pamoja na mameneja wa Mikoa na vituo wa Wakala huo ambapo amewataka kuhakikisha wanajiimarisha ili kuendelea kutoa huduma bora na zinazokidhi viwango. Akizungumza katika Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa TEMESA Mkoa wa Dodoma Waziri Kamwelwe amewataka kutekeleza maagizo yote ambayo ameyatoa ikiwemo kupunguza gharama za matengenezo ya magari, kununua vipuri kwa wingi pamoja na kuhakikisha mafundi wanapatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuendana na teknolojia ya kisasa ya ufundi wa magari.