KIVUKO KIPYA CHA MV. ILEMELA CHAFANYIWA MAJARIBIO

Kivuko kipya cha MV.Ilemela leo kimefanyiwa majaribio na kushuhudiwa na mamia ya wakazi wa Wilaya ya Ilemela akiwemo Mbunge wa jimbo hilo Dkt.Angelina Mabula. Kivuko hicho kilifanya safari kutokea Yadi ya Songoro kuelekea Kayenze na baadae kwenda katika kisiwa cha Bezi ambako kote huko kilipokelewa kwa shangwe na mamia ya wakazi wa visiwani humo ambao hawakusita kuonyesha furaha yao kutoka a na ujio wa kivuko hicho. Kivuko cha MV.Ilemela kimerejea katika yadi mara baada ya majaribio hayo na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya taratibu zote kukamilika.