KIVUKO KIPYA CHA KAYENZE BEZI (MV.ILEMELA) CHASHUSHWA KWENYE MAJI

Wakazi wa Ilemela mkoa wa Mwanza leo wameshuhudia kwa mara ya kwanza kivuko kipya cha Kayenze Bezi, MV.Ilemela ambacho kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.7 kikishushwa kwenye maji baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Kivuko cha MV.Ilemela kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.