VIVUKO VYA BILIONI 7.3 KUKAMILIKA FEBRUARI MWAKANI

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatarajiwa kukamilisha ujenzi wa vivuko viwili vipya vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 ifikapo mwezi Februari mwaka 2020. Hayo yamebainishwa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Profesa Idrissa B. Mshoro alipotembelea yadi ya Songoro Ilemela jijini Mwanza kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko hivyo unaoendelea katika karakana hiyo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alialikwa kushuhudia ukaguzi huo.