SERIKALI YAZINDUA RASMI UJENZI WA VIVUKO VIWILI UKARA NA CHATO

SERIKALI imezindua rasmi ujenzi wa vivuko vipya viwili vya kisasa vitakavyotoa huduma ya kusafirisha abiria , mizigo na magari kati ya Bugorola-Ukara Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza na Chato-Nkome Wilaya ya Chato mkoani Geita. Uzinduzi huo umefanyika mkoani Mwanza katika eneo la karakana ya Kampuni ya Songoro Marine Transport Boaty Ltd, inayojenga vivuko hivyo ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Chato na Ukerewe walihudhuria hafla hiyo.