WAZIRI KAMWELWE AKAGUA ENEO LA MRADI WA UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MAFIA NYAMISATI

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amefanya ziara kukagua eneo la mradi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Mafia Nyamisati. Mradi huo ambao unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.3 za kitanzania ambapo kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200, magari 6 sawa na Tani 100, . Zoezi hili limefanyika katika yadi ya Songoro iliyopo katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam.