KIKAO CHA WADAU MKOANI ARUSHA

Mkoani Arusha, kikao cha wadau kimefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College), Mgeni rasmi wa kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha ndugu David Mwakiposa aliupongeza wakala kwa kuweza kuandaa kikao hicho ili kuweza kupata changamoto na ushauri kutoka kwa wadau inayowahudumia. Aliushauri wakala kuendelea kutoa huduma bora ili kuendelea kuzivutia taasisi mbalimbali za watu binafsi kuanza kutumia huduma za TEMESA. ''Lazima tutumie huduma za TEMESA na wale waliopewa dhamana hiyo wawe tayari kutoa huduma iliyo bora wakati wote, hiyo itasaidia kuwavutia wale ambao hawatumii huduma zetu'', alisema Katibu Tawala.