SERIKALI YASHUSHA KIVUKO CHA BILIONI 4.2 UKARA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) leo imefanikiwa kurejesha faraja ya wakazi wa visiwa vya Bugorola na Ukara baada ya kuzindua kivuko kipya kilichogharimu shilingi bilioni 4.2, MV.UKARA II (HAPA KAZI TU). Kivuko hicho kipya ambacho kimejengwa na mkandarasi mzawa Songoro Marine Transport ya jijini Mwanza kina uwezo wa kubeba abiria 300 na magari 10 ambazo ni sawa na tani 100.