MTENDAJI MKUU TEMESA APOKEA KIVUKO CHA MV ILEMELA-MWANZA

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) umepokea Kivuko cha MV Ilemela kilichotengenezwa kwa gharama ya Sh.bilioni 2.7 zilizotolewa na Serikali ya Tanzania. Kivuko hicho kilitengenezwa na Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ya jijini Mwanza ambapo kilianza kujengwa Aprili mwaka jana na kukamilika Februari 6, mwaka huu na kuingizwa majini kwa ajili ya kufanyiwa majaribio. Akizungumza leo wakati wa mapokezi wa Kivuko hicho,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle alisema kwamba kivuko hicho kitaanza kazi rasmi ya kubeba abiria kutoka Kayenze kwenda kisiwa cha Bezi kwa gharama ya Shilingi 1000.