VIVUKO TEMESA VYAJIIMARISHA KUZUIA CORONA

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupitia Vivuko vyake vyote nchini imeendelea kujidhatiti kwa kuhakikisha hakuna ongezeko la maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoambukizwa na virusi vya Corona (Covid-19). Vivuko vyote vimeendelea kuhakikisha vinatoa elimu kwa watumishi wa Vivuko pamoja na abiria wanaotumia Vivuko hivyo kwa kufuata kanuni na taratibu za afya kwa ajili ya kujikinga na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi hivyo.