MAFIA NYAMISAT FERRY CONSTRUCTION REACHES 98 PERCENT

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Mv. Kilindoni Hapa Kazi Tu kitakachokuwa kinafanya safari kati ya kisiwa cha Mafia na Nyamisati umefikia asilimia 98 na kwamba ifikapo Desemba 15 mwaka huu kitaingia majini kwa mara ya kwanza. ’’Wana-Mafia tumekuwa tukizungumza sana sasa tumefikia hatua kwamba kivuko chetu kimeshakamilika bado asilimia mbili ambazo ni kazi ndogo na haya ni matokeo ya mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana.’’