TEMPORARY EMPLOYMENT DODOMA

Posted On Thursday 19th Dec , 2019

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA)

TANGAZO LA KAZI

KAZI YA MUDA

Kumb. Na.AE.228/244/01/90 16 DISEMBA, 2019

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) niTaasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria Na 30 ya mwaka 1997. Majukumu yake makubwa ni kutoa huduma za matengenezo ya magari na mitambo, huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya taa za barabarani, kufanya matengenezo ya majokofu, viyoyozi na kufanya matengenezo ya mifumo ya TEHAMA na vifaa vya kielektroniki, kutoa huduma za vivuko na huduma za ushauri.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA, katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda kama ifuatavyo:

1.Msaidizi wa Ofisi – Nafasi 3

  • (a)Sifa za mwombaji:
  • i.Awe na elimu ya kidato cha nne aliyefaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.

(b) Majukumu

i.Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki na kusafisha vyoo.

ii.Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

iii.Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.

iv.Kutayarisha chai ya Ofisi.

v.Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka posta.

vi.Kuhakikisha vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili.

vii.Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya saa za kazi.

viii.Kudurufu barua na machapisho kwenye mashine za kudurufia.

ix.Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.

x.Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.

  • MASHARTI YA JUMLA

(i)Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa Watumishi wa Umma.

(ii)Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania.

(iii)Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti husika, picha mbili ndogo za rangi (passport size) za mwombaji, cheti cha kuzaliwa na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.

(iv)Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.

(v)Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 02 Januari, 2020.

(vi)Barua za maombi zitumwe kwa:

Mtendaji Mkuu,

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),

Jengo la PSSSF,

Ghorofa ya Nane,

Barabara ya Makole,

S.L.P. 1075,

DODOMA.