TEMPORARY EMPLOYMENT

Posted On Thursday 3rd Sep , 2020

TANGAZO LA KAZI

KAZI YA MUDA

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria Na 30 ya mwaka 1997. Majukumu yake makubwa ni kutoa huduma za matengenezo ya magari na mitambo, huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya taa za barabarani, kufanya matengenezo ya majokofu, viyoyozi na kufanya matengenezo ya mifumo ya TEHAMA na vifaa vya elektroniki, kutoa huduma za vivuko na huduma za ushauri.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda katika vituo vya “Mobile Workshops” kwenye mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara, Tabora, Mbeya na Karakana ya Same iliyoko mkoani Kilimanjaro kama ifuatavyo;

1.Fundisanifu Magari/Mitambo (Motor Vehicle Mechanics/AutomobileTechnician)Daraja la II – Nafasi 14

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na elimu ya kidato cha sita na kuhitimu kozi ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

ii.Awe na elimu ya kidato cha nne na kufuzu kozi ya miaka mitatu katika fani ya Ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

iii.Awe na elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Majaribio ya Ufundi Stadi Hatua ya I (Trade Test I) fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

iv.Awe Raia wa Tanzania.

v.Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) wa kufanya matengenezo ya magari madogo na makubwa /mitambo kwenye karakana /gereji iliyosajiliwa

vi.Awe mchapakazi, anayejiamini na mwenye uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa.

vii.Mwenye uzoefu kwenye matengenezo ya magari /mitambo ya kisasa atapewa kipaumbele.

(b) Majukumu

i.Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya magari na mitambo.

ii.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

iii.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

iv.Kufanya usafi wa karakana, vifaa na mazingira yake.

v.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 2. Fundisanifu Umeme wa Magari (Auto-Electric Technician)Daraja la II – Nafasi 6
  • (a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na elimu ya kidato cha sita na kuhitimu kozi ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ufundi Umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

ii.Awe na elimu ya kidato cha nne na kufuzu kozi ya miaka mitatu katika fani ya Ufundi umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

iii.Awe na elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua ya I (Trade Test I) katika fani ya Ufundi umeme magari/mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

iv.Awe Raia wa Tanzania.

v.Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) wa kufanya matengenezo ya mifumo ya umeme/elektroniki kwenye magari madogo na makubwa/mitambo kwenye karakana/gereji iliyosajiliwa.

vi.Awe mchapakazi, anayejiamini na mwenye uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa.

vii.Mwenye uzoefu kwenye matengenezo ya mifumo ya umeme/elektroniki ya magari /mitambo ya kisasa atapewa kipaumbele.

(b)Majukumu

i.Kuchunguza na kubaini matatizo ya mifumo ya umeme

na elektroniki kwenye magari/mitambo na kuyatatua.

ii. Kufanya matengenezo ya vifaa vya umeme/elektroniki

kwenye magari/mitambo

iii.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

iv.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

v. Kufanya usafi wa eneo la kazi na mazingira yake.

vi.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

MASHARTI YA JUMLA

(i)Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45.

(ii)Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne.

(iii)Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania.

(iv)Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti husika, picha mbili ndogo za rangi (passport size) za mwombaji, cheti cha kuzaliwa na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.

(v)Mwombaji anatakiwa kutaja jina la kituo anachoombea kazi kwenye barua ya maombi ya kazi

(vi)Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.

Aidha, Usaili utafanyika TEMESA Makao Makuu Dodoma Kwa Watakao kuwa na sifa. Hatahivyo, ofisi haitahusika na gharama zozote kwa mwombaji ikiwa ni pamoja na nauli,chakula,malazi n.k.

(vii)Barua za maombi zitumwe kwa:

Mtendaji Mkuu,

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),

S.L.P. 1075

DODOMA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA TAREHE 02/09/2020

N.B. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 16/09/2020