TEMPORARY EMPLOYMENT

Posted On Thursday 25th Jun , 2020


TANGAZO LA KAZI

KAZI YA MUDA

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) niTaasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria Na 30 ya mwaka 1997. Majukumu yake makubwa ni kutoa huduma za matengenezo ya magari na mitambo, huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya taa za barabarani, kufanya matengenezo ya majokofu, viyoyozi na kufanya matengenezo ya mifumo ya TEHAMA na vifaa vya elektroniki, kutoa huduma za vivuko na huduma za ushauri.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme, katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda kama ifuatavyo:

 • 1.AFISA TEHAMA – NAFASI 1
 • (a)Sifa za mwombaji:
 • i.Awe na cheti cha kidato cha nne
 • ii.Awe na Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika mojawapo ya fani zifuatazo: Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.
 • (b)Majukumu
 • i.Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa Kompyuta (Design, install and configure LAN and WAN infrustructure,
 • ii.Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa Kompyuta (Test network equipment and divices),
 • iii.Kusimamia utekelezaji wa alama za mtandao wa Kompyuta (Implement network security) maelekezo ya usalama wa mtandao kwa mujibu wa miongozo ya “usty guidelines”,
 • iv.Kutathmini na kurekebisha hitilafu zozote za mtandao wa Kompyuta (Perform network troubleshooting and repair), na
 • v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.

MASHARTI YA JUMLA

 • i.Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa Watumishi wa Umma.
 • ii.Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti husika, picha mbili ndogo (passport size) za mwombaji na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.
 • iii.Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.
 • iv.Barua za maombi zitumwe kwa:

MTENDAJI MKUU,

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME,

S.L.P. 1075,

DODOMA.

N.B. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 03/07/ 2020