TEMPORARY EMPLOYMENT

Posted On Wednesday 27th May , 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA)

TANGAZO LA KAZI

KAZI YA MUDA

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) niTaasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria Na 30 ya mwaka 1997. Majukumu yake makubwa ni kutoa huduma za matengenezo ya magari na mitambo, huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya taa za barabarani, kufanya matengenezo ya majokofu, viyoyozi na kufanya matengenezo ya mifumo ya TEHAMA na vifaa vya elektroniki, kutoa huduma za vivuko na huduma za ushauri.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme, katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda kama ifuatavyo:

1. Dereva (Magari) – nafasi 2

 • (a)Sifa za mwombaji:
 • i.Awe na Cheti cha Kidato cha nne, Leseni daraja la “E” au “C1” ya uendeshaji magari ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali
 • ii.Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye cheti Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
 • (a)Majukumu
 • i.Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
 • ii.Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
 • iii.Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
 • iv.Kukusanya na Kusambaza nyaraka mbalimbali.
 • v.Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
 • vi.Kufanya usafi wa gari; na
 • vii.Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wako.

MASHARTI YA JUMLA

 • i.Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa Watumishi wa Umma.
 • ii.Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti husika, picha mbili ndogo (passport size) za mwombaji na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.
 • iii.Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.
 • iv.Barua za maombi zitumwe kwa:

MTENDAJI MKUU,

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME,

S.L.P. 1075,

DODOMA.

N.B. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05/06/2020