TANGAZO LA KAZI ZA MUDA

Imewekwa Monday 11th Dec , 2023

TANGAZO LA KAZI

KAZI ZA MUDA

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala wa Serikali Sura ya 245. Majukumu yake makubwa ni kutoa Huduma za Matengenezo ya Magari na Mitambo, Huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya Matengenezo ya Taa za Barabarani, kufanya Matengenezo ya Majokofu, Viyoyozi na kufanya Matengenezo ya Mifumo ya TEHAMA na Vifaa vya Elektroniki, kutoa Huduma za Vivuko na Huduma za Ushauri.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda kama ifuatavyo:

  • 1.MHASIBU DARAJA LA II – NAFASI5

(a)Sifa za mwombaji:

Mwenye Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani zifuatazo: Uhasibu, Fedha, Usimamiziwa Biashara aliyejiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Fedha, au wenye "Intermediate Certificate" (Module D) inayotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo kutoka katika Taasisi inayotambuliwa na Serikali pamoja na CPA (T), ACCA, ACA, CIA au sifa zinazolingana na hizo za kitaaluma zinazotambuliwa na NBAA .

(b)Majukumu

i. Kuandaa taarifa za mapato na matumizi na ripoti zinazohusiana;

ii. Kupokea mapato ya TEMESA na kuweka sawa katika Benki kwa wakati;

iii. Kufanya usuluhishi wa Akaunti za Benki na masuala mengine ya kifedha

yanayohusiana nayo;

iv. Kufanya ukaguzi na ukaguzi wa awali wa hati za malipo na

v. Kufanya kazi zozote atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.

  • 2.AFISA HESABU DARAJA LA II – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

Mwenye Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani zifuatazo: Uhasibu, Fedha, Usimamiziwa Biashara aliyejiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Fedha, au wenye "Intermediate Certificate" (Module D) inayotolewa na NBAAau sifa zinazolingana na hizo kutoka katika Taasisi inayotambuliwa na Serikali .

(b)Majukumu

i. Kuandaa taarifa za malipo, ratiba na orodha mbalimbali za matumizi mbalimbali;

ii.Kutunza “vote book” na rejesta mbalimbali (k.m. wadaiwa, masurufu,

wadai);

iii.Kutumika kama keshia kwa fedha zinazopokea na kulipa, kutoa risiti za

fedha zilizopokelewa na kupata kibali cha fedha zilizolipwa;

iv.Kuweka na kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya benki ya TEMESA

na kuandaa taarifa za usuluhishi wa benki;

v.Kutunza hesabu za leja, jarida, kitabu cha fedha na rekodi nyingine za uhasibu na kuoanisha hesabu za udhibiti katika leja kuu na Leja tanzu;

vi.Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na msimamizi wake

wa kazi.

  • 3.MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

Mwenye Astahahada katika mojawapo ya fani zifuatazo: Uhasibu, Fedha,

Usimamiziwa Biashara aliyejiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Fedha au sifa zinazolingana na hizo kutoka katika Taasisi inayotambuliwa na Serikali auATEC I zinazotolewa na NBAA

(b)Majukumu

i.Kuweka nyaraka za Uhasibu kwenye mafaili husika

ii.Kupanga faili zinazohusu shughuli za uhasibu katika sehemu za kuhifadhi.

iii. Kutuma hundi kwa wanaolipwa.

iv. Kutayarisha hati za malipo.

v. Kutoa risiti za fedha zilizopokelewa na kupata kibali cha fedha zilizolipwa

vi. Kuhifadhi rejista ya mali za kudumu na kuhakikisha kuwa inahuishwa

kila wakati

vii. Kuhifadhi rekodi za “staff imprest” na retirements”

viii. Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na msimamizi wake

wa kazi.

MASHARTI YA JUMLA

i.Mwombaji awe ni raia wa Tanzania.

ii.Barua za maombi ziambatishwe na nakala za vyeti husika pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa, picha mbili ndogo (passport size) za mwombaji na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.

iii.Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.

Barua za maombi zitumwe kwa:

Mtendaji Mkuu,

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA),

S. L. P. 1075,

DODOMA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA TAREHE 11 Desemba, 2023

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 24 Desemba, 2023