TANGAZO

Posted On Wednesday 17th Jul , 2019

TAARIFA KWA UMMA

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA) UNAPENDA KUUJULISHA UMMA KUWA UMEFUNGUA RASMI KARAKANA YA WILAYA KATIKA MJI WA IFAKARA ITAKAYO HUDUMIA WILAYA ZA KILOMBERO, ULANGA NA MALINYI PAMOJA NA MAENEO YA JIRANI.

HUDUMA ZOTE ZA WAKALA ZINAPATIKANA KATIKA KARAKANA HIYO IKIWEMO MATENGENEZO YA MAGARI, PIKIPIKI, MITAMBO, MIFUMO YA UMEME WA MAJENGO, MAJOKOFU, VIYOYOZI NA TEHAMA KWA OFISI ZOTE ZA SERIKALI NA TAASISI ZAKE PAMOJA NA WATU BINAFSI.

OFISI ZA TEMESA ZINAPATIKANA KATIKA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA MAENEO YA KIBAONI UJENZI.

KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI YETU www.temesa.go.tz NA MITANDAO YETU YA KIJAMII TWITTER, FACEBOOK NA INSTAGRAM @temesatanzania AU PIGA SIMU NAMBA 0759-931 055 NA 0712- 784 282

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MASOKO NA UHUSIANO

TEMESA