TAARIFA KWA UMMA

Imewekwa Wednesday 1st Feb , 2023

TAARIFA KWA UMMA

UKARABATI WA MV MAGOGONI

Ili kupata mkandarasi atakayefanya ukarabati mkubwa wa MV. MAGOGONI, Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ulifuata taratibu za manunuzi za ushindanishi wa Kimataifa (International Competitive Tendering) ili kupanua wigo wa ushindani. Matokeo ya mchakato huu ni kwamba kampuni ya kizalendo ilishika namba mbili ikiwa na gharama zaidi kwa shilingi za kitanzania 2.5 bilioni kulinganisha na mshindi wa kwanza. Hivyo wakala ulimpatia kazi hiyo mkandarasi aliyeshika namba moja katika mchakato huo.

Aidha, mkandarasi aliyeshinda zabuni hii anao uwezo na uzoefu mkubwa wa kazi hizi unaojumuisha matengenezo ya meli na boti zinazomilikiwa na Serikali pamoja na makampuni binafsi hapa Tanzania.

USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI

Tayari viongozi wakubwa wa Kitaifa wametoa maelekezo kuitaka TEMESA ishirikiane na Sekta binafsi ili kuongeza ufanisi na kuipunguzia Serikali mzigo wa uendeshaji. Katika kulitekeleza hili TEMESA imekamilisha uandaaji wa mkakati wa maboresho (TEMESA Transformation Strategy) ambao unapendekeza mabadiliko ya muundo, sheria na unaweka mkazo katika ushirikiano na sekta binafsi. Aidha, TEMESA inakamilisha andiko la fursa za uwekezaji zilizopo ili kuutangazia Umma na kukaribisha watu binafsi wenye nia na uwezo wa kuwekeza.

Imetolewa na Kitengo cha Masoko na Uhusiano

TEMESA