TAARIFA KWA UMMA

Imewekwa Monday 28th Feb , 2022

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSIMAMA KUTOA HUDUMA KIVUKO CHA MV. KAZI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) anawatangazia wananchi wote wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni kuwa kivuko cha MV. KAZI kimeondolewa kwenye maji Tarehe 20 Februari 2022 na kupelekwa kufanyiwa matengenezo makubwa baada ya muda wake wa kufanyiwa matengenezo hayo kuwa umefika.

Huduma za uvushaji abiria na mizigo zinaendelea kama kawaida kwa kutumia vivuko vya MV. KIGAMBONI na MV. MAGOGONI kwa kipindi chote cha matengenezo husika.

Aidha TEMESA inawashauri watumiaji wa kivuko hasa wale wanaovuka na magari kutumia Daraja la Nyerere ili kuepusha msongamano.

TEMESA inawaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano

20/02/2022