TANGAZO LA KAZI

Imewekwa Tuesday 14th Mar , 2023

TANGAZO LA KAZI

KAZI ZA MUDA

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala wa Serikali Sura ya 245. Majukumu yake makubwa ni kutoa Huduma za Matengenezo ya Magari na Mitambo, Huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya Matengenezo ya Taa za Barabarani, kufanya Matengenezo ya Majokofu, Viyoyozi na kufanya Matengenezo ya Mifumo ya TEHAMA na Vifaa vya Elektroniki, kutoa Huduma za Vivuko na Huduma za Ushauri.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda kama ifuatavyo:

  • 1.FUNDISANIFU DARAJA LA II (UMEME WA MAGARI) – NAFASI 5
  • (a)Sifa za mwombaji:

i.Awe amehitimu kidato cha sita na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ufundi wa Umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

ii.Awe amehitimu kidato cha nne na kufuzu kozi ya miaka mitatu katika fani ya ufundi wa Umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

iii.Awe na elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Majaribio ya Ufundi Stadi Hatua ya I (Trade Test I) au “Level III” au “Certificate Three” katika fani ya ufundi Umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au

iv.Awe na elimu ya kidato cha nne na Stashahada ya Kawaida katika fani ya Ufundi Umeme wa Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

v.Awe uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi wa magonjwa ya magari katika eneo la umeme wa magari

  • (b)Majukumu

i.Kuchunguza na kubaini matatizo ya mifumo ya umeme na elektroniki kwenye magari/mitambo na kuyatatua.

ii.Kufanya matengenezo ya vifaa vya umeme/elektroniki kwenye magari/mitambo

iii.Kufanya uchunguzi, kubaini, kuandaa gharama na kurekebisha matatizo ya umeme katika magari kwa kutumia mashine za utambuzi wa magonjwa ya magari katika eneo la umeme wa magari

iv.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

v.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

vi.Kuhakikisha vifaa vya karakana na mazingira yake ni safi wakati wote.

vii.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 2.FUNDISANIFU DARAJA LA II (MITAMBO/MAGARI) – NAFASI 5
  • (a)Sifa za mwombaji:

i. Awe amehitimu kidato cha sita na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

ii. Awe amehitimu kidato cha nne na kufuzu kozi ya miaka mitatu katika fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

iii. Awe na elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Majaribio ya ufundi Stadi Hatua ya I (Trade Test I) au “Level III” au “Certificate Three” katika fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au

iv. Awe na elimu ya kidato cha nne na Stashahada ya Kawaida katika fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

v. Awe na uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi wa magonjwa ya magari katika eneo la magari

(a) Majukumu

  • i.Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya magari na mitambo.
  • ii.Kufanya uchunguzi, kubaini, kuandaa gharama na kurekebisha matatizo ya magari na Mitambo
  • iii.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi
  • iv.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.
  • v.Kuhakikisha vifaa vya karakana na mazingira yake ni safi wakati wote.
  • vi.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
  • 3.FUNDISANIFU DARAJA LA II (UMEME) – NAFASI 5
  • (a)Sifa za mwombaji:

i. Awe amehitimu kidato cha sita na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya ufundi Umeme kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

ii. Awe amehitimu kidato cha nne na kufuzu kozi ya miaka mitatu katika fani ya ufundi Umeme kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, au

iii. Awe na elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Majaribio ya ufundi Stadi Hatua ya I (Trade Test I) au “Level III” au “Certificate Three” katika fani ya ufundi Umeme kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au

iv. Awe na elimu ya kidato cha nne na Stashahada ya Kawaida katika fani ya ufundi Umeme kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

v. Awe uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi wa matatizo ya umeme

(a)Majukumu

i.Kufanya matengenezo ya vifaa vya umeme

ii.Kufanya upimaji wa Umeme kufuatana na maelekezo ya Mhandisi

iii.Kufanya usanifu wa miradi midogo ya umeme

iv.Kufanya uchunguzi, kubaini, kuandaa gharama na kurekebisha matatizo ya mifumo ya umeme kwa kutumia mashine za utambuzi wa matatizo ya umeme

v.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

vi.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

vii.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi

  • 4.FUNDISANIFU MSAIDIZI (UMEME WA MAGARI) – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na elimu ya kidato cha nne katika masomo ya sayansi na kufuzu masomo ya mwaka mmoja katika fani ya ufundi wa Umeme wa Magari kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali. au:

ii.Awe na elimu ya kidato cha nne mwenye cheti cha majaribio ya ufundi hatua ya II au “Level II” au “Certificate Two” kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya Umeme wa Magari.

iii.Awe uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi wa magonjwa ya magari katika eneo la umeme wa magari

(b) Majukumu

i.Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya umeme wa magari na mitambo.

ii.Kuchunguza na kubaini matatizo ya mifumo ya umeme na elektroniki kwenye magari/mitambo na kuyatatua.

iii.Kufanya matengenezo ya vifaa vya umeme/elektronikikwenye magari/mitambo

iv.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

v.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

vi.Kufanya usafi wa eneo la kazi na mazingira yake.

vii.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 5.FUNDISANIFU MSAIDIZI (MITAMBO/ MAGARI) – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na elimu ya kidato cha nne katika masomo ya sayansi na kufuzu masomo ya mwaka mmoja katika fani ya ufundi Magari/Mitambo kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali. au

Awe na elimu ya kidato cha nne mwenye cheti cha majaribio ya ufundi hatua ya II au “Level II” au “Certificate Two” kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya Magari/Mitambo.

ii. Awe na uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi wa magonjwa ya magari katika eneo la magari

(b)Majukumu

i.Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya magari na mitambo.

ii.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

iii.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

iv.Kuhakikisha vifaa vya karakana na mazingira yake ni safi wakati wote.

v.Kufanya uchunguzi, kubaini na kurekebisha matatizo ya magari

vi.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 6.FUNDISANIFU MSAIDIZI (UMEME )- NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na elimu ya kidato cha nne katika masomo ya sayansi na kufuzu masomo ya mwaka mmoja katika fani ya ufundi wa Umeme kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali. au:

ii.Awe na elimu ya kidato cha nne mwenye cheti cha majaribio ya ufundi hatua ya II au “Level II” au “Certificate Two” kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya Umeme.

iii.Awe uwezo na uzoefu wa kutumia mashine za utambuzi na matatizo ya umeme

(b)Majukumu

i.Kufanya matengenezo madogo na makubwa ya umeme.

ii.Kuchunguza na kubaini matatizo ya mifumo ya umeme na kuyatatua.

iii.Kufanya matengenezo ya vifaa vya umeme

iv.Kuhakikisha usalama kwa watumishi na mali wakati wote wa utendaji kazi

v.Kuhifadhi na Kutunza vifaa anavyofanyia kazi.

vi.Kufanya usafi wa eneo la kazi na mazingira yake.

vii.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 7.AFISA UGAVI MSAIDIZI – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Kuajiriwa wenye Stashahada ya Ununuzi/Ugavi au Biashara iliyojiimarisha katika Ununuzi na Ugavi, kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali, au sifa inayolingana na hizo inayotambuliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement andSupplies Professionals and Technicians Board - (PSPTB).

ii.Awe amesajiliwa na PSPTB kama Procurement and Supplies Technician" au "Procurement and Supplies Full Technician"

iii.Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

(a)Majukumu

i.Kutunza na kupanga vifaa vilivyomo ghalani katika hali ya usafi na usalama.

ii.Kupokea vifaa vilivyonunuliwa kutoka kwa wazabuni.

iii.Kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

iv.Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.

v.Kufungua leja (Ledger) ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka ghalani.

vi.Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

vii.Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

  • 8.MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA I – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

  • AU

ii.Awe na Cheti cha ATEC II inayotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinayotambulika na NBAA.

(b)Majukumu

i.Kutunza daftari Ia fedha Ia matumizi ya kawaida na maendeleo.

ii.Kutunza nyaraka za hati za malipo.

iii. Kuingiza mapato na matumizi kwenye vitabu vya fedha.

iv.Kuandika taarifa mbalimbali za fedha zilizopokelewa.

v. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake

wa kazi

9.AFISA TEHAMA – NAFASI 3

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika mojawapo ya fani zifuatazo: Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.

  • (a)Majukumu

i.Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa Kompyuta (Design, install and configure LAN and WAN infrustructure,

ii.Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa Kompyuta (Test network equipment and divices),

iii.Kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya usalama wa mtandao kwa mujibu wa miongozo ya usalama wa mtandao wa Kompyuta (Implement network security guidelines),

iv.Kutathmini na kurekebisha hitilafu zozote za mtandao wa Kompyuta (Perform network troubleshooting and reparair), na

v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.


  • 10.MWANDISHI MWENDESHA OFISI/ KATIBU MAHSUSI DARAJA LA II –
  • NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe amehitimu Kidato cha Nne wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au mwenye cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha awe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E- mail na Publisher kutoka Chuo chochote inachotambuliwa na Serikali.

(b)Majukumu

i.Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri;

ii.Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu

iii.wanapoweza kushughulikiwa;

iv.Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wako na ratiba ya kazi zingine Mkuu wako na ratiba ya kazi zingine;

v.Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;

vi.KupokeamajaladanakusambazakwaMaofisawalio katika ldara/Kitengo/Sehemu husika;

vii.Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyarakasehemu inazohusika;

viii.Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;

ix.Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi;

x.Kuanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 11.MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 5

(a)Sifa za mwombaji:

i.Awe na stashahada ya (NTA Level 6) katika fani ya masjala, wenye ujuzi wa kompyuta kutoka chuo kinachotambulika na Serikali

  • .

(b)Majukumu

i.Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (incoming correspondence register);

ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoing correspondence register)

iii.Kusambaza majalada kwa watandaji (action officers)

iv.Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji

v.Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;

vi.Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.

vii.Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)

viii.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

  • 12.DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5
  • (a)Sifa za mwombaji:

    i.Awe na Cheti cha Kidato cha nne, Leseni daraja la “E” au “C1” ya uendeshaji magari ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali

    ii.Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye cheti Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

    (b)Majukumu

    i.Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa

    • gari.

    ii.Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

    iii.Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari

    iv.Kukusanya na Kusambaza nyaraka mbalimbali.

    v.Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari

    vi.Kufanya usafi wa gari; na

    vii.Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake wa kazi.

    • 13.DEREVA VIVUKO DARAJA LA II - NAFASI 5

    (a)Sifa za mwombaji:

    i.Awe na elimu ya kidato cha nne

    ii.Awe na ujuzi wa kuendesha na kutunza Kivuko uliothibitishwa na chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili. (Rating of Navigation Watch/Refresher Rating au “Class Four with COC,”

    iii.Awe amefuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye Vivuko (Mandatory courses /Refresher in mandatory courses).

    (b) Majukumu

    i.Kuendesha na kuongoza Kivuko;

    ii.Kutoa maelekezo ya kufunga na kufungua kamba za Kivuko;

    iii.Kusimamia usalama wa abiria na mizigo ndani ya Kivuko;

    iv.Kusimamia upangaji wa abiria na mizigo kwenye Kivuko;

    v.Kuhakikisha kwamba injini ya Kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi;

    vi.Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi;

    vii.Kutunza daftari la safari za Kivuko;

    viii.Kutunza nyaraka muhimu za Kivuko;

    ix.Kusimamia nidhamu na utendaji wa watumishi walio chini yake;

    x.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

    • 14.BAHARIA – NAFASI 5

    (a)Sifa za mwombaji:

    i.Awe na Cheti cha Kidato cha nne,

    ii.Awe na ujuzi wa kutunza kivuko/mashua uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Institute au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili (Rating Forming Part of Navigation Watch) au “Class Four with COC,”

    iii.Awe amefuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini/kuogelea na kupanga watu na magari kwenye vivuko/mashua (Mandatory Courses).

    (b)Majukumu

    i.Kufunga na kufungua kamba za vivuko/mashua.

    ii.Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya vivuko/mashua.

    iii.Kupanga abiria na magari kwenye kivuko/mashua

    iv.Kutunza daftari la safari za vivuko/mashua.

    v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

    • 15.WAZAMIAJI (DIVERS) – NAFASI 5

    (a)Sifa za Mwombaji:

    i.Awe na Elimu ya Kidato cha Nne

    ii.Awe amesomea kozi ya Uzamiaji/Uokoaji “Diver PADI” na uzoefu wa kazi usipungua miaka miwili (2)

    iii.Awe amefuzu mafunzo ya miezi sita ya Kozi za Uokoaji wa Maisha majini na Kuogelea (Mandatory Courses zifuatazo “Fire Prevention and Fire Fighting, Elementary First Aid, Personal Safety and Social Responsibilities, Personal Survival Techniques “) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

    (b)Majukumu:

    i.Kupiga mbizi, kukagua na kusafisha mara kwa mara mifumo ya uendeshaji ya vivuko (Pump Jet/Propeller) iliyo ndani ya maji ili iweze kufanya kazi inavyotakiwa kuzuia uharibifu;

    ii.Kusaidia katika shughuli za Uokoaji (pale inapotokea ajali au mali imezama kwenye maji);

    iii.Kuhakikisha kwamba takataka zinazotokea karibu na maeneo ya vivuko na njia za vivuko zinaondolewa kuzuia uharibifu wa mifumo ya uendeshaji wa kivuko;

    iv.Kukagua na kuchunguza umbo la kivuko chini ya maji na matenki ya vivuko “Hull bottom area and compartments” zinakuchunguzwa mara kwa mara kama zinaingiza maji na mapungufu yote yanaripotiwa kwa ukarabati;

    v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa Kazi

    • 16.MCHUMI DARAJA LA II – NAFASI 1

    (a)Sifa za Mwombaji:

    i.Mwenye Shahada ya Kwanza katika moja ya fani zifuatazo; Uchumi,Mipango na Usimamizi wa Miradi, Uchumi na Fedha, Takwimu, Uchumi na Takwimu au sifa zinazolingana na hizo kutoka kwa taasisi zinazotambulika.

    (b) Majukumu:

    i.Kuandaa bajeti ya Wakala;

    ii.Kufanya utafiti juu ya fursa za masuala ya sera za kiuchumi;

    iii.Kuandaa mbinu za ukusanyaji wa takwimu za masuala mbalimbali

    ya Wakala; programu za uendeshaji;

    iv.Kuratibu maandalizi ya Mipango Kazi ya TEMESA;

    v.Kuratibu na kutoa maoni kuhusu mwenendo wa matumizi ya

    kawaida ya Wakala;

    vi.Kuandaa bajeti, mpango kazi na mpango kazi wa Wakala;

    vii.Kutayarisha uandishi wa mradi na

    viii.Kufanya kazi nyingine zozote zinazohusiana kama itakavyoagizwa

    mara kwa mara na msimamizi.

    • 17. AFISA UHUSIANO WA UMMA DARAJA LA II -NAFASI 1

    (a)Sifa za mwombaji:

    i.Wenye Shahada ya Kwanza katika moja ya fani zifuatazo; Uandishi wa habari, Mawasiliano ya Umma, Mahusiano ya Kimataifa, Mahusiano ya Umma au sifa zinazolingana na hizo kutoka kwa taasisi zinazotambulika.

    (b)Majukumu

    i.Kusaidia katika kuwezesha makongamano, semina, sherehe n.k;

    ii.Kusaidia katika utayarishaji wa vipindi vya Redio na TV;

    iii.Kutunza kumbukumbu za picha za matukio makubwa;

    iv.Kudumisha, kusasisha na kupakia tovuti ya Wakala kwa ushirikiano na mtaalamu wa TEHAMA;

    v.Kuratibu taarifa na malalamiko ya mteja kwa njia ya bila malipo, rejesta na kutoa taarifa kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma;

    vi.Kuongoza na kusindikiza wageni rasmi kwenye ofisi na mitambo ya

    Mamlaka; na

    vii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa Kazi

    MASHARTI YA JUMLA

    i.Mwombaji awe ni raia wa Tanzania.

    ii.Barua za maombi ziambatishwe na nakala za vyeti husika pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa, picha mbili ndogo (passport size) za mwombaji na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.

    iii.Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.

    Barua za maombi zitumwe kwa:

    Mtendaji Mkuu,

    Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA),

    S. L. P. 1075,

    DODOMA.

    TANGAZO HILI LIMETOLEWA TAREHE 13 MACHI 2023

    MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 26 MACHI, 2023