TANGAZO LA KAZI
Imewekwa Thursday 26th Jan , 2023
TANGAZO LA KAZI
KAZI ZA MUDA
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala wa Serikali Sura ya 245. Majukumu yake makubwa ni kutoa Huduma za Matengenezo ya Magari na Mitambo, Huduma za Umeme ikiwa ni pamoja na kufanya Matengenezo ya Taa za Barabarani, kufanya Matengenezo ya Majokofu, Viyoyozi na kufanya Matengenezo ya Mifumo ya TEHAMA na Vifaa vya Elektroniki, kutoa Huduma za Vivuko na Huduma za Ushauri.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), katika kuhakikisha kuwa majukumu ya Wakala yanatekelezwa anatangaza nafasi za kazi za muda katika Makao Makuu ya Wakala kama ifuatavyo:
- 1.KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III – NAFASI 2
- (a)Sifa za mwombaji:
i.Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu Mtihani wa hatua ya Tatu.Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahilina Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepatamafunzo yaKompyutakutoka Chuo chochotekinachotambuliwa na Serikalina kupata chetikatika program za Window Microsoft Office, Internet, E.mail na Publisher.
ii. Mwenye uzoefu wa miaka miwili (2) ya kazi katika fani hii atafikiriwa kwanza.
- (b)Majukumu
i.Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
ii.Kuhakikisha Lugha na huduma nzuri zinazotolewa kwa Wateja wa Ndani na Nje ya Ofisi.
iii.Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanya kazi, na kumuarifu Mkuu wako kwa wakati unaohitajika.
iv.Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyarakaau kitu chochote kinachohitajikakatika shughuli za kazi hapo ofisini.
v.Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasadizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozoteanazokuwa amepewana wasaidizi hao.
vi.Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maafisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii.Kuhakikisha kuwa Siri za Ofisi (Nyaraka na Taarifa mbalimbali) hazitoki kwa wasiohusika/mhusika pasipo idhini ya Mwenye Mamlaka.
viii.Kuhakikisha vifaa vya ofisi (Kompyuta) viko sehemu salama.
ix.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
- 2.MPOKEZI – NAFASI 1
- (a)Sifa za mwombaji:
i.Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati, na kufuzu mafunzo ya Mapokezi ya Upokeaji simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
ii.Mwenye uzoefu wa miaka miwili (2) ya kazi katika fani hii atafikiriwa kwanza.
- (b)Majukumu
i.Kupokea wageni na wasaili shida zao.
ii.Kutunza rejesta ya wageni za ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni, wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
iii.Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
iv.Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
v.Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakaopewa huduma.
vi.Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wana miadi (appointment) au wamepata idhini ya maafisa husika.
vii.Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisambalimbali ofisini .
viii.Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
ix.Kutunza rejesta ya simu zinazopokolewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
- x.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
MASHARTI YA JUMLA
i.Mwombaji awe ni raia wa Tanzania.
ii.Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45.
iii.Barua za maombi ziambatishwe na nakala za vyeti husika pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa, picha mbili ndogo (passport size) za mwombaji na taarifa binafsi (curriculum vitae) ya mwombaji.
iv.Waombaji watakaokuwa na sifa zinazohitajika ndio watakaoitwa kwenye usaili.
Barua za maombi zitumwe kwa:
Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA),
S. L. P. 1075,
DODOMA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA TAREHE 25/01/2023.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 07/02/2023.