HOTUBA YA MAKADIRIO YA BAJETI 2023/24

Imewekwa Monday 22nd May , 2023

MUHTASARI WA HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHESHIMIWA PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

A.UTANGULIZI

  • 1.Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,

naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/24.

  • 2.Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana leo.
  • 3.Mheshimiwa Spika, naomba kuungana na Bunge lako Tukufu katika kumpongeza kwa dhati Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutimiza miaka miwili katika kutuongoza kwa umahiri na mafanikio makubwa.
  • 4.Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais kwa namna anavyomsaidia Mheshimiwa Rais katika kuongoza nchi yetu.
  • 5.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri na

makini.


  • 6.Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kukupongeza wewebinafsikwakazikubwaunayoifanyayakusimamiana

kuliongoza Bunge letu Tukufu kwa weledi mkubwa. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), Naibu Spika kwa kuendelea kutekeleza vyema shughuli za Bunge. Vilevile, nichukue fursa hii kuwapongeza Wenyeviti Wote wa Bunge kwa kuchaguliwa kwao. Tunawaahidi ushirikiano katika kutimiza wajibu wa kusimamia na kuliongoza Bunge letu.

  • 7.Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima, ninaomba nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini katika kutekeleza majukumu yangu nikiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi tangualiponiteuatarehe12Septemba,2021.Ninaomba

kumhakikishia kuwa, nitaendelea kutekeleza majukumu yangu kwa uwezo na uaminifu mkubwa ili kuliletea Taifa letu maendeleo. Ninamuahidi kuwa nitatumia weledi, maarifa na uwezo wangu wote katika kutekeleza wajibu wangu kwa ufanisi mkubwa.

  • 8.Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nimpongeze Mheshimiwa Selemani Moshi Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge

ya Miundombinu na Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati. Aidha, nawapongeza Wajumbe wote walioteuliwa kwenye Kamati hii. Nichukue fursa hii kuishukuru Kamati hii kwa kuendelea kutoa ushauri na kuisimamia Wizara.


  • 9.Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kutoa salamu za pole kwa Bunge lako Tukufu na wote walioguswa na kifo cha Mbunge mwenzetu Mhe. Mussa Hassan Mussa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo

la Amani, Zanzibar. Tutaendelea kuthamini na kuuenzi mchango wake katika Bunge hili na Taifa kwa ujumla. Aidha, nimpongeze Mhe. Abdul Yussuf Maalim kwa kuaminiwa na wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo la Amani.

  • 10.Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba sasa nitoe taarifa ya mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi na maombi

ya fedha kwa mwaka wa fedha 2023/24.

B.MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23

  • 11.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imegawanywa katika mafungu mawili kibajeti ambayo ni Fungu 98

(Sekta ya Ujenzi) na Fungu 62 (Sekta ya Uchukuzi). Nitaanza na maelezo kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa Sekta ya Ujenzi ikifuatiwa na Sekta ya Uchukuzi.


B-1: SEKTA YA UJENZI

Bajeti ya Matumizi ya Kawaida

  • 12.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Ujenzi ilitengewa jumla ya Shilingi Bilion 44.293 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi Aprili, 2023 jumla ya Shilingi Bilion 32.893, sawa naasilimia74.26yafedhazilizoidhinishwanaBungezilikuwa

zimetolewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Bajeti ya Miradi ya Maendeleo

  • 13.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Ujenzi ilitengewa Shilingi Trilioni 1.377. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi Trilioni 1.124 fedha

za ndani na Shilingi Bilioni 252.965 fedha za nje. Fedha za ndani kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Funds) ni Shilingi Bilioni 777.785 na kutoka Mfuko wa Barabara ni Shilingi Bilioni 599.756.

Hadi Aprili, 2023 fedha zilizopokelewa ni Shilingi Trilioni 1.312 sawa na asilimia 95.3 ya fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2022/23. Kati ya fedha hizi, Shilingi Trilioni 1.069 ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni 243.321 ni fedha za nje.

  • 14.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuipongeza na kuishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. SamiaSuluhuHassankwakuendeleakulipahatizamadaiya

Makandarasi na Washauri Elekezi kwa wakati.


Aidha, kutokana na malipo hayo kufanyika kwa wakati, kasi ya utekelezaji wa miradi imeongezeka. Vilevile tunaishukuru sana Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwalipa Makandarasi na Washauri Elekezi ambapo katika mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya Shilingi 184.459 zimetolewa kwa ajili ya malipo ya madeni.

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Miradi ya Barabara na Madaraja

  • 15.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, miradi ya barabara kuu iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 470 pamoja na ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 33.

Kazi nyingine ni kuendelea na ujenzi wa madaraja makubwa manne

(4): Daraja la Kigongo – Busisi, Mwanza; Daraja la Gerezani (Dar es Salaam), Daraja la Pangani (Tanga) na Daraja la Wami (Pwani).

  • 16.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2023, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 179.18 umekamilika na ujenzi wa kilometa 290.82 unaendelea. Aidha, ujenzi wa madaraja

makubwa mawili (2) ya Wami na Gerezani umekamilika. Vilevile, ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi, Mwanza umefikia asilimia 72 na ujenzi wa daraja la Pangani (Tanga) umefikia asilimia 3.

  • 17.Mheshimiwa Spika, miradi ya barabara za mikoa iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/23 ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 103.01. Kazi nyingine

ni kufanya ukarabati kwa kiwango cha changarawe wa barabara zenye urefu wa kilometa 1,042.43.

  • 18.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2023 jumla ya kilometa 23.11 za barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 253.67 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe.

Miradi ya Barabara na Madaraja Iliyokamilika

  • 19.Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio katika eneo la ujenzi wa barabara na madaraja.

Katika kipindi chake cha miaka miwili wa uongozi wa Mheshimiwa Rais, barabara katika maeneo mbalimbali zimejengwa na kukamilika. Barabara hizo ni pamoja na:-

i).Barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu (km 201); Sehemu ya Waso – Sale Jct (km 49) mkoani Arusha;

ii).Barabara ya Morocco – Mwenge (km 4.3) kutoka Njia tano hadi Sita (km 3.2) Mkoani Dar es Salaam;

iii).Barabara ya Kongwa Jct – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 98); Sehemu ya Mbande – Kongwa Jct (km 5.80) Mkoani Dodoma;

iv).Barabara ya Tabora – Koga – Mpanda; Sehemu ya 3: Kasinde – Mpanda (km 108) pamoja na kipande cha Barabara ya Urwira (km 3.7) Mkoani Katavi;


v).Barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi (km 268); Sehemu za Kidahwe – Kasulu (km 63) na Kakonko – Nyakanazi (km 50) Mkoani Kigoma;

vi).Barabara ya Bulamba – Kisorya (km 51) Mkoani Mara; vii).Barabara ya Makutano – Nyamuswa – Ikoma Gate (km 153);

Sehemu ya Makutano – Sanzate (km 50) Mkoani Mara;

viii).Barabara ya Musoma – Makojo – Busekela; Sehemu ya Kuseni – Suguta (km 5) Mkoani Mara;

ix).Barabara ya Chunya – Makongorosi (km 39) Mkoani Mbeya; x).Barabara ya Mtwara – Newala – Masasi (km 210); Sehemu ya

Mtwara – Mnivata (km 50) Mkoani Mtwara;

xi).Barabara ya Njombe – Ndulamo – Makete (km 107.4) Mkoani Njombe;

xii).Barabara ya Itoni – Ludewa – Manda; Sehemu ya Lusitu – Mawengi (km 50) Mkoani Njombe;

xiii).Barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 112) Mkoani Rukwa;

xiv).Barabara ya Masasi – Songea Mbamba Bay; Sehemu ya Mbinga – Mbamba Bay (km 66) Mkoani Ruvuma;

xv).Barabara ya Mpemba – Isongole (km 50.3) Mkoani Songwe; xvi).Barabara ya Urambo – Kaliua – Ilunde – Uvinza; Sehemu ya

Urambo – Kaliua (km 28) Mkoani Tabora;

xvii).Barabara ya Manyoni – Itigi – Tabora; Sehemu ya Nyahua – Chaya (km 85) Mkoani Tabora; na


xviii).Barabara ya Tabora – Koga – Mpanda; Sehemu Usesula – Komanga (km 108) pamoja na Sehemu ya Komanga - Kasinde (km 108) pamoja na Inyonga Spur (km 4.8).

  • 20.Mheshimiwa Spika, Aidha, kuna miradi mbalimbali mikubwa ya ujenzi wa barabara inayoendelea na iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa:
  • i).Barabara ya Mianzini – Olemringaringa – Ngaramtoni Juu na Olemringaringa – Sambasha/Timbolo (km 18) – Kazi za ujenzi zinaendelea na zimefikia asilimia 18 Mkoani Arusha;
  • ii).Upanuzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha kuwa Njia Nane (8 lanes), (km 19.2) na Madaraja matatu ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji Mkoani Dar es Salaam;
  • iii).Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka; Awamu ya Pili (BRT Phase II) (km 19.3) na Awamu ya Tatu (Phase III): Nyerere Road corridor kutoka CBD - Gongolamboto (km 23.33) Mkoani Dar es Salaam;
  • iv).Barabara za Mzunguko wa Nje Jijini Dodoma (Dodoma City Outer Ring Roads); Sehemu ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.30) (Lot 1) na Sehemu ya Ihumwa – Dry Port – Matumbulu – Nala (Km 60.00) (Lot 2) Mkoani Dodoma;
  • v).Barabara ya Kumunazi – Bugene – Kasulo na Kyaka – Mutukula (km 124); Sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60); Mkoani Kagera;
  • vi).Barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260.0); sehemu za Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5); Mvugwe – Nduta Junction (km 59.35); Kibondo Junction – Kabingo (km 62.5); Nduta Junction – Kibondo (km 25.9) na Kasulu – Manyovu pamoja na barabara za kuingia Kasulu mjini (km 68) mkoani Kigoma;

  • vii).Barabara ya Kazilambwa – Chagu (km 36) mkoani Kigoma;
  • viii).Barabara ya Malagarasi – Ilunde – Uvinza (km 51.1); Mkoani Kigoma;
  • ix).Barabara ya Dumila – Kilosa; Sehemu ya Ludewa – Kilosa (km 18) mkoani Morogoro;
  • x).Barabara ya Mikumi – Kidatu – Ifakara; Sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 66.9): Mkoani Morogoro;
  • xi).Barabara ya Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389); Sehemu ya Mbulu – Garbabi (km 25) Mkoani Manyara;
  • xii).Barabara ya Tarime – Mugumu (km 87.14); Sehemu ya Tarime – Nyamwaga (Lot 1: Mogabiri - Nyamongo) (km 25) Mkoani Mara;
  • xiii).Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba (km 56.4) Mkoani Mara;
  • xiv).Barabara ya Itoni – Ludewa – Manda, Mkoani Njombe;
  • xv).Barabara ya Tanga – Pangani – Mkange; Sehemu ya Tanga – Pangani (km 50) na Sehemu ya Tungamaa – Mkange (km 95.2)

Mkoani Tanga; na

  • xvi).Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kwamtoro – Singida (km 434.33) Sehemu ya Handeni – Mafuleta (km 20): Ujenzi unaendelea na umefikia asilimia 11; Sehemu ya Mafuleta – Kileguru (km 30): Taratibu za manunuzi kwa ajili ya ujenzi zinaendelea.

  • 21.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa ujenzi wa madaraja jumla ya madaraja makubwa nane (8) yamejengwa na kukamilika ambayo ni:
  • i).Daraja la Wami (Pwani),
  • ii).Daraja la Tanzanite (DSM),
  • iii).Daraja la Gerezani (DSM),
  • iv).Daraja la Mpwapwa (Dodoma),
  • v).Daraja la Kiegeya (Morogoro),
  • vi).Daraja la Ruhuhu (Ruvuma),
  • vii).Daraja la Kitengule (Kagera) na
  • viii).Daraja la Msingi (Singida).

Miradi ya Barabara, Madaraja na Viwanja vya Ndege Iliyosainiwa Mwaka wa Fedha 2022/23

  • 22.Mheshimiwa Spika, mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege ilisainiwa katika mwaka wa fedha 2022/23. Miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za

Lusahunga – Rusumo (km 92); Kitulo – Iniho (km 36.3); Sengerema – Nyehunge (km 54); Utete – Nyamwage (km 33.7); Kibondo – Mabamba (km 48); Igawa – Songwe – Tunduma Sehemu ya Uyole – Ifisi - Airport (km 32); Ibanda – Itungi Port (km 26); Kajunjumele – Kiwira Port (km 6); Barabara unganishi katika daraja la Sibiti (km 24.83) na barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa sehemu ya Noranga – Doroto (km 6) na Itigi – Mkiwa (km 25.569). Miradi mingine ni ujenzi wa Madaraja ya Mpiji Chini na Mbambe. Aidha, mikataba ya miradi ya ujenzi wa Viwanja vya Ndege iliyosainiwa ni ya viwanja vya ndege vya Kigoma na Sumbawanga. Utekelezaji wa

miradi hii uko katika hatua za maandalizi ya kuanza kazi.


Miradi ya Barabara Itakayojengwa kwa Utaratibu wa EPC+F

  • 23.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara ilianza taratibu za manunuzi kwa ajili ya kuwapata Makandarasi wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara saba (7) zenye jumla ya kilometa 2035 kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F). Barabara hizi zitafungua fursa za kiuchumi katika maeneo zinapopita na kwa Taifa kwa ujumla.

Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Makandarasi wa miradi yote saba

(7) wamepatikana na mikataba ya kazi za ujenzi inatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023. Barabara ambazo zitajengwa kwa utaratibu huu wa EPC + F ni: -

  • i).Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435);
  • ii).Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (Simiyu) (km 339);
  • iii).Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijochini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 460);
  • iv).Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa Junction (km 453.42);
  • v).Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175);
  • vi).Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (km 218) pamoja na barabara ya mchepuo ya Uyole – Songwe yenye urefu wa kilometa 48.9, na
  • vii).Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81).

  • 24.Mheshimiwa Spika, hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kuwa na miradi mikubwa yenye jumla ya kilometa 2,035 ambayo

itaanza kutekelezwa kwa wakati mmoja katika maeneo mbalimbali nchini na itagharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 3.7.

  • 25.Mhe. Spika haya ni maoni na maelekezo ya Mhe. Dr. Samia

Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Mungano wa Tanzania kwa ya kutaka kuifungu nchi kwa haraka sana. Munamshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mradi ya Barabara Itakayotekelezwa kwa Utaratibu wa PPP

  • 26.Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP), Wizara inaendelea na manunuzi ya makandarasi kwa ajili ya

ujenzi wa Expressway kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Hadi sasa kazi inayoendelea ni uchambuzi (evaluation) wa Makandarasi walioonesha nia (Expression of Interest) ya kutekeleza mradi huu kwa sehemu ya kutoka Kibaha – Chalinze yenye urefu wa kilometa 78.9. Kwa sehemu ya Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 126.1, Mshauri Elekezi anaendelea na kazi ya Upembuzi Yakinifu.

  • 27.Mheshimiwa Spika, hii itakuwa ni mara yakwanza katika

historia ya nchi yetu kuwa na mradi mkubwa hapa nchini ambao utatekelezwa kwa utaratibu wa PPP.

(Utekelezaji wa miradi ya Barabara na Madaraja umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 7 hadi 43)


Viwanja vya Ndege,

  • 28.Mheshimiwa Spika, TANROADS imeendelea kutekeleza miradi ya uendelezaji wa viwanja vya ndege, ambapo ukarabati na upanuzi

wa Viwanja vya Ndege vya Songea na Mtwara umekamilika. Aidha, kazi za ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege pamoja na eneo la usalama (Runway End Safety Area-RESA), usimikaji wa taa za usalama na taa za kuongozea ndege (AGL) katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe zimekamilika. Kwa sasa, Mkandarasi anaendelea na kazi ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 98.

  • 29.Mheshimiwa Spika, Kazi ya ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Sumbawanga, Shinyanga, Tabora na Kigoma

umeanza na Makandarasi wako kwenye hatua za maandalizi (mobilization).

  • 30.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, hadi Aprili, 2023 utekelezaji wa Package I unaohusisha ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege

(runway), barabara za maungio (taxiway), maegesho ya ndege (apron), uzio wa usalama, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani (access roads), maegesho ya magari (car parking) na usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege (AGL) umefikia asilimia 18. Aidha, utekelezaji wa Package II unaohusisha ujenzi wa jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, kituo cha zimamoto, kituo cha hali ya hewa na


vituo vidogo nane (8) vya kufua umeme unaendelea na umefikia asilimia 2. Kuhusu Kiwanja cha Ndege cha Musoma, kazi ya upanuzi na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio na uzio wa usalama inaendelea na utekelezaji umefikia asilimia 47.

Utekelezaji wa miradi ya Viwanja vya Ndege UMEONESHWA kuanzia ukurasa wa 51 hadi 54.

  • 31.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) iliendelea kutekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa VIVUKO na maegesho ya vivuko katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Utekelezaji wa kina wa miradi ya ukarabati, ununuzi na ujenzi wa vivuko, hadi Aprili, 2023, umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 45 hadi 47.

  • 32.Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya Serikali katika mwaka wa fedha

2022/23.

Utekelezaji wa kina wa MIRADI WA Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 47 hadi 49.


Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2023 utendaji wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi: kuanzia Bodi ya Mfuko wa Barabara, Wakala ya Majengo Tanzania, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadsiriaji Majenzi, Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Baraza la Taifa la Ujenzi, Kituo cha Usambazaji wa Tecknoloji Katika Sekta ya Ujenzi na Usafirishaji umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 54 hadi 67

B-2:SEKTA YA UCHUKUZI (FUNGU - 62)

Bajeti iliyoidhinishwa na fedha zilizotolewa kwa mwaka 2022/23

Bajeti ya Matumizi ya Kawaida

  • 33.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Uchukuzi iliidhinishiwa Shilingi Bilion 94.546 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi kufikia Aprili, 2023 jumla ya Shilingi Bilion 71.955 sawa na asilimia 76.11 zilikuwa zimetolewa.

Bajeti ya Maendeleo

  • 34.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Sekta ya Uchukuzi iliidhinishiwa Shilingi Trilioni 2.041 kwa ajili ya utekelezaji

wa Miradi ya Maendeleo. Hadi kufikia Aprili, 2023 jumla ya Shilingi Trilioni 1.847 sawa na asilimia 90.51 zilikuwa zimetolewa.


UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NA UTOAJI HUDUMA

Udhibiti wa Usafiri kwa Njia ya Barabara

  • 35.Mheshimiwa Spika, Udhibiti wa Usafiri wa Barabara unatekelezwanaMamlakayaUdhibitiUsafiriArdhini(LATRA).

Mamlaka hiyo inadhibiti utoaji wa huduma za usafiri wa kibiashara kwa abiria na mizigo ikijumuisha mabasi, malori, teksi, pikipiki za magurudumu matatu na za magurudumu mawili.

(Utendaji wa udhibiti wa usafiri kwa njia ya barabara umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu katika ukurasa wa 69 hadi 74).

Huduma za Usafiri kwa Njia ya Reli Shirika la Reli Tanzania (TRC)

  • 36.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara inaendelea na ujenzi wa Awamu ya Kwanza ya mradi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza (Km 1,219) uliogawanyika katika vipande vitano (5). Hadi kufikia Aprili, 2023 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa kwa kipande cha Dar es Salaam -

Morogoro (Km 300) ni asilimia 98.14; Morogoro - Makutupora (Km 422) asilimia 93.83; Mwanza - Isaka (Km 341) asilimia 31.07; Makutupora - Tabora (Km 368) asilimia 7; na Tabora - Isaka (Km 165) asilimia 2.39.


  • 37.Mheshimiwa Spika, katika Hotuba ya mwaka 2022/23, tuliahidi kuanza maandalizi ya ujenzi wa awamu ya pili ya reli ya Standard

Gauge (SGR). Napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa, Serikali imeanza ujenzi wa Reli ya SGR kwa awamu ya pili katika kipande cha Tabora – Kigoma (Km 506) ambapo imesaini mkataba na Kampuni ya CCECC na CRCC kutoka China na kwa sasa Mkandarasi anakamilisha maandalizi ya ujenzi. Utendaji na Utekelezaji wa miradi ya reli kupitia TRC umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 74 hadi 78).

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)

  • 38.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), hadi kufikia Aprili 2023, TAZARA ilisafirisha jumla ya tani 244,492 za mizigo na jumla ya abiria 765,706

wa njia ndefu. Utendaji wa TAZARA umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 78 hadi 80.

Udhibiti wa Huduma za Usafiri kwa njia ya Maji

  • 39.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendelea kusimamia ulinzi na usalama wa

vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za usafiri majini.

  • 40.Mheshimiwa Spika,TASAC inaendelea kusimamia ujenzi wa Kituo kikuu cha Uratibu wa shughuli za Utafutaji na Uokoaji cha kikanda kitakachojengwa eneo la Ilemela Mwanza.

Kwa sasa Mkandarasi tayari amekabidhiwa eneo kwa ajili ya kuanza shughuli za ujenzi na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane (18). Vilevile, mkandarasi amepatikana kwa ajili ya kujenga vituo vingine vidogo 3 vya utafutaji na uokoaji katika maeneo ya Kanyala (Geita), Nansio (Ukerewe) na Musoma (Mara) na kwa sasa maandalizi ya ujenzi yanaendelea. Utendaji wa udhibiti wa huduma za usafiri wa kwa njia ya maji na utekelezaji wa miradi umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 80 hadi 84.

Huduma za Uchukuzi Katika Maziwa Makuu

  • 41.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imeendelea kutoa huduma za usafiri na usafirishaji

kwenye Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Hadi Aprili, 2023 MSCL ilisafirisha abiria 170,137 na tani za mizigo 18,909.

  • 42.Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa meli zinazotoa huduma katika Maziwa Makuu. Hadi Aprili, 2023 ujenzi wa meli mpya ya MV.

Mwanza ulifikia asilimia 83; Ukarabati wa meli ya MV Umoja ulifikia asilimia 75.8 na Ukarabati wa MT Sangara ulifikia asilimia 90.7.

Aidha, Serikali kupitia MSCL ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na Mkandarasi ili kuwezesha kuanza ujenzi wa meli mbili

(2) katika Ziwa Tanganyika; Meli moja (1) katika Ziwa Victoria na Chelezo katika Ziwa Tanganyika.


Hatua iliyofikiwa ya ukarabati ya MV Liemba hadi sasa ni kuwa Makandarasi amepatikana na mkataba ya kazi za ukarabati wa meli hiyo inatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023. Kazi ukarabati itafanyika kwa miezi tisa (9). Pia, kazi ya matengenezo ya utulivu (stability) ya MV Muongoza itaanza hivi karibuni. Utendaji na utekelezaji wa miradi MSCL umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 85 hadi 87).

Huduma za Bandari

  • 43.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ilihudumia shehena ya tani milioni 20.851 na makasha 765,504. Aidha, TPA inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Bandari za Mwambao na za Maziwa Makuu. Mradi

wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam imefikia asilimia 96. Aidha, kwa Bandari ya Tanga, TPA imekamilisha Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Bandari hiyo kwa kuimarisha na kuboresha Gati Na. 1 na 2 zenye urefu wa mita 450 ambapo mradi umekamilika kwa asilimia 99. Kwa upande wa Bandari za Maziwa makuu, ujenzi wa Bandari ya Karema umekamilika na imeanza kutumika. Aidha, ujenzi wa gati, ghala la kuhifadhia makaa ya mawe, jengo la abiria, ofisi na sehemu ya kuegesha meli (ramp) katika Bandari ya Ndumbi Ziwa Nyasa umekamilika. Utendaji na utekelezaji wa miradi ya TPA umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 87 hadi 95.


Udhibiti wa Huduma za Usafiri kwa Njia ya Anga

  • 44.Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kutoa huduma za udhibiti wa usafiri wa anga, viwanja vya ndege, masuala ya kiusalama na kiuchumi katika huduma za usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji

ndege katika viwanja 14 nchini. Utendaji na utekelezaji wa miradi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga unaonyeshwa katika kitabu cba hutuba ya bujeti kuanzia ukurasa wa 95 hadi 100.

Huduma za Viwanja vya Ndege

  • 45.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya NdegeTanzania(TAA)inajukumulakusimamia,kuendesha,

kuboresha na kuendeleza viwanja vya ndege 58 vinavyomilikiwa na Serikali.

  • 46.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TAA imekamilisha maandalizi ya mahitaji ya kiufundi na ununuzi wa kandarasi kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya abiria katika viwanja vya ndege vya Mpanda, Songea, na

Kahama. Pia. imeanza maandalizi ya ujenze wa Jengo la Waongoza Ndege katika Kiwanja cha Ndege Bukoba. Pia TAA imeanza matayarisho ya ukamilisha wa ujenzi wa Jengo la Abiria wa Kiwanja cha ndege cha Mwanza.


  • 47.Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2023, kazi ya uwekaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ili kiweze kutumika kwa saa 24 imefikia asilimia 40.
  • 48.Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa shughuli za uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

(KIA) chini Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Wizara inaendelea na taratibu za kutunga Sheria mahsusi ya TAA kwa ajili ya kuwezesha Viwanja vyote vya Ndege nchini, ikiwemo KIA, kuwa chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Tanzania. Utekelezaji wa majuku ya Viwanja vya Ndege umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 101 hadi 107.

Huduma za Usafiri kwa Njia ya Anga

  • 49.Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na juhudi za kuimarisha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Juhudi hizo ni pamoja na kuendelea na usimamizi wa utengenezaji wa ndege mpya

nne (4) ambazo ni Boeing 767-300F moja (1) ya mizigo inayotarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi Mei, 2023; Ndege 2 za Boeing 737-9 zinazotarajiwa kuwasili mwezi Agosti na Disemba, 2023; na Ndege 1 ya Boeing 787-8 Dreamliner inayotarajiwa kuwasili mwezi Februari, 2024. Kutokana na mpango wa Serikali wa kuongeza ndege mpya nne (4), ATCL inatarajia kupanua wigo wa safari zake kwa kuongeza vituo vipya sita (6) vya nje na 3 vya ndani.


Utendaji wa utoaji huduma za usafiri na Usafirishaji kwa njia ya anga umeainishwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 107 hadi 110.

HUDUMA ZA HALI YA HEWA

  • 50.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kutekeleza mradi wa kununua na kufungaRadanne(4)zahaliyahewa.Radambili(2)tayari

zimeshapokelewa na kazi ya ufungaji inaendelea katika mikoa ya Mbeya na Kigoma na Rada nyingine mbili (2) zitakazofungwa mkoani Dodoma na Kilimanjaro zinatarajiwa kuwasili mapema mwakani. Utendaji na utekelezaji wa miradi ya huduma za hali ya hewa umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 111 hadi 113.

TAASISI ZA MAFUNZO

  • 51.Mheshimiwa Spika, Utendaji WA Taasisi za Mafunzo zilizo chini ya WIZARA (sekta ya Uchukuzi) umeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 113 hadi 121.

C.CHANGAMOTOZILIZOIKABILIWIZARANAMIKAKATIYA KUZITATUA

  • 52.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekabiliwa na changamoto mbalilimbali katika utekelezaji wa majukumu yake. Changamoto hizo na mikakati ya kuzitatua zimeoneshwa katika Kitabu cha Hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 137 hadi ukurasa

wa 142.


D.MPANGONAMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

  • 53.Mheshimiwa Spika, Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2023/24 umeandaliwa kwa kuzingatia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano na Ilani ya

Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 pamoja na maelekezo ya Serikali. Makadirio ya Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo kwa Sekta ya Ujenzi na Sekta ya Uchukuzi ni kama ifuatavyo:-

D - 1: SEKTA YA UJENZI (FUNGU – 98)

Makadirio ya Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo

  • 54.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/24, Sekta ya Ujenzi imetengewa Shilingi Bilion 48.395 ikiwa ni Bajeti ya Matumizi ya Kawaida. Aidha, Bajeti ya Maendeleo kwa mwaka 2023/24 ni Shilingi Trilion 1.419. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilion 1.084 ni fedha za ndani na Shilingi Bilion 335.176 ni za fedha za nje. Kati ya

fedha za ndani Shilingi Bilion 599.756 ni fedha kutoka Mfuko wa Barabara na fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali ni Shilingi Bilioni 484.909.

Mgawanyo wa fedha za maendeleo pamoja na miradi iliyotengewa fedha ni kama inavyooneshwa katika Kiambatisho Na. 1 na Na. 2.


  • 55.Mheshimiwa Spika,

VIPAUMBELE VYA MPANGO NA BAJETI YA SEKTA YA UJENZI

  • (i)Kuanza ujenzi wa miradi saba (7) ya barabara yenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineeering Procurement Construction and Finance ( EPC + F).
  • (ii)Kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro Expressway yenye urefu wa kilometa 205 kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP).
  • (iii)Kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara katika maeneo mbalimbali yenye jumla ya urefu wa kilometa 1,031.98.
  • (iv)Kuendelea na Miradi ya Ujenzi wa Barabara iliyosaniwa Katika Mwaka wa Fedha 2022/23 yenye jumla ya urefu wa kilometa 393.6
  • (v)Kuendelea na ujenzi wa madaraja makubwa mawili (2) ya JPM (Kigongo – Busisi, Mwanza) na Pangani (Tanga) pamoja na kujenga madaraja mengine katika maeneo mbalimbali nchini.
  • (vi)Kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 269.12 ambazo zinatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2022/23.
  • (vii)Kuendelea na utekelezaji wa mradi ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato pamoja na Kuendelea na kazi za ukarabati na upanuzi wa viwanja vingine vya ndege katika mikoa mbalimbali.

  • 56.Mheshimiwa Spika, Miradi yote hiyo ya barabara na madaraja ikamilikaitakuwanajumlayakilometa3,934.7zabarabara

zilizojengwa kwa lami ambazo zitaongeza urefu wa mtandao wa barabara za lami zilizopo sasa za kilometa 11,587.82 na kufikia kilometa 15,522.52 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 34.

D - 2:SEKTA YA UCHUKUZI (FUNGU – 62)

Makadirio ya Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo

  • 57.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/24, Sekta ya Uchukuzi (Fungu 62) imetengewa jumla ya Shilingi Trilioni 2.086 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 118.215 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi Trilioni 1.968 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Mgawanyo wa fedha za maendeleo pamoja na miradi iliyotengewa fedha imeovyooneshwa katika Kiambatisho Na. 6.

  • 58.Mheshimiwa Spika, VIPAUMBELE VYA MPANGO NA BAJETI YA SEKTA YA UJENZI
  • i.Mradi wa Kuwezesha Taasisi (Institutional Support) – Shilingi bilioni 18.3;
  • ii.Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa Victoria – Shilingi bilioni 1.73;
  • iii.Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam – Shilingi bilioni 93.80.
  • iv.Miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Reli (RIF)- Shilingi bilioni 294.80;

  • v.Mradi wa Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli Iliyopo (MGR) – Mradi wa Tanzania Intermodal Railway II – Shilingi bilioni 11.72;
  • vi.Mradi wa Ujenzi wa Reli Mpya ya Standard Gauge Shilingi trilioni 1.113;
  • vii.Mradi wa Ununuzi wa Rada, Vifaa na Ujenzi wa Miundombinu ya Hali ya Hewa – Shilingi bilioni 13.00;
  • viii.Mradi wa Uboreshaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) – Shilingi bilioni 300.00;
  • ix.Mradi wa Ujenzi wa Meli Mpya na Ukarabati wa Meli –

Shilingi bilioni 100.00;

  • x.Mradi wa Kuboresha Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia – Shilingi bilioni 2.27;
  • xi.Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya TAZARA- Shilingi bilioni

13.19; na

  • xii.Mradi wa Ununuzi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege na Uendelezaji wa Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga – Shilingi bilioni 6.5.

E.SHUKRANI

  • 59.Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena nichukue fursa hii kuwapongezanakutambuamchangomkubwaunaotolewana

viongozi wenzangu katika kutekeleza majukumu ya Wizara yangu, nikianzia na Naibu Mawaziri, Mheshimiwa Mhandisi Godfrey Kasekenya na Mheshimiwa Fred Mwakibete; Makatibu Wakuu, Balozi Mhandisi Aisha Salim Amour (Ujenzi) na Ndugu Gabriel Joseph Migire (Uchukuzi); Naibu Makatibu Wakuu Ndugu Ludovick


James Nduhiye (Ujenzi) na Dkt. Ally Saleh Possi (Uchukuzi). Vilevile, kipekee napenda kuishukuru Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watumishi wote wa Wizara na Taasisi kwa jitihada zao katika utekelezaji wa Majukumu ya Wizara.

  • 60.Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wizara naomba kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati na kuwatambua wadau wote wa Wizara ikiwa ni pamoja na Washirika mbalimbali wa Maendeleo ambao

wamechangia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa Programu, Miradi na Mipango mbalimbali ya Wizara. Aidha, napenda kuwatambua wafuatao: Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga, Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini, Shirika la Hali ya Hewa Duniani, UNESCO, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia, Japan (JICA), OPEC Fund, Korea Kusini (KOICA), Abu Dhabi Fund, Ujerumani (KfW), Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Shirika la Maendeleo la Marekani, Kuwait (KFAED), HSBC, TMEA, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za SADC, Dubai, China, Denmark, Norway, Ubelgiji, Ujerumani na Uturuki, Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi za fedha zote za kifedha nchini na Asasi mbalimbali zisizokuwa za Serikali; Sekta Binafsi pamoja na wadau wengine wengi ambao sitamaliza endapo nitawataja wote.

  • 61.Mheshimiwa Spika, naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwako wewe binafsi Mhe. Naibu Spika na kwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.HotubahiipiainapatikanakatikatovutiyaWizara

(www.mwt.go.tz).na info@temesa.go.tz


FMUHTASARI WA MAOMBI YA FEDHA YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI KATIKA MWAKA WA FEDHA 2023/24

  • 62.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/24, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 3,554,783,957,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,468,238,449,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na Shilingi 2,086,545,508,000.00nikwaajiliyaSektayaUchukuzi.

Mchanganuo wa fedha zinazoombwa kwa kila Fungu ni kama ifuatavyo:

SEKTA YA UJENZI (FUNGU 98)

  • 63.Mheshimiwa Spika, Shilingi 1,468,238,449,000.00 za Fungu 98 (Ujenzi) zinajumuisha Shilingi 48,395,392,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 1,419,843,057,000.00 ni kwa ajili ya

Bajeti ya Maendeleo.

SEKTA YA UCHUKUZI (FUNGU 62)

  • 64.Mheshimiwa Spika, Sekta ya Uchukuzi inaombewa jumla ya Shilingi 2,086,545,508,000.00. Kati ya hizo, Shilingi 118,215,599,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi

1,968,329,909,000.00 ni kwa ajlili ya Miradi ya Maendeleo.

  • 65.Mheshimiwa Spika, pamoja na Hotuba hii, nimeambatisha Miradi ya Wizara itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/24 kuanzia Kiambatisho Na. 1 – 6. Naomba viambatisho hivyo vichukuliwe kama sehemu ya vielelezo vya hoja hii.
  • 66.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.